P&L

P&L

MANISPAA YA UBUNGO YAPITISHA BAJETI YA BILIONI 98.2, YATAJA VIPAUMBELE 17


Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo iliyopo Jijini Dar es Salaam limepitisha bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/19 ambapo imekadiria kutumia kiasi cha Sh. bilioni 98.2 .

Akifafanua matumizi ya fedha hizo, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amesema katika fedha hizo kiasi cha Sh. 76,607,163,700 ni matumizi ya kawaida na mishahara ya watumishi ambayo ni sawa na asilimia 78 ya Bajeti yote. Wakati Sh 21,631,029,900 ni fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo sawa na asilimia 22 ya bajeti yote.

Vile vile, Meya Jacob amesena wamekidhi kigezo cha kutenga asilimia 60 ya fedha za mapato ya ndani katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ambayo ni Sh.12,600,760,400.00 na Sh. 8,498,717,600 iliyo sawa na asilimia 40 zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na mishahara.

Akifafanu zaidi wakati anasoma bajeti hiyo Jacob amesoma vipaumbele 17 vya Halmashauri kwa mwaka 2018/2019.

Ametaja vipaumbele hivyo ni ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Sh bilioni 3, uboreshaji wa mfumo wa ukusanyaji mapato ya ndani, kukusanya Sh.bilioni 25.7

Pia miradi ya maendeleo imetengewa fedha kiasi cha Sh.billioni 21.6 wakati kipaumbele cha nne kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa kununua dawa na vifaa tiba Sh.bilioni 8.2.

Jacob ametaja kipaumbele cha tano ni kupandisha maslahi ya wajumbe Serikali za Mitaa kutoka sh. 5000 kwa mwezi mpaka sh 20,000 kwa mwezi.

Pia kuboresha miundombinu ya barabara kwa viwango vya lami,matengenezo ya kawaida,kujenga madaraja na makalvati na vivuko vya waenda kwa miguu, fedha kiasi cha Sh.bilioni 1.4 zimetengwa kupelekwa TARURA.

Jacob amesena kipaumbele cha saba ni uenzi wa viwanda vidogovidogo na uwekezaji,fedha kiasi cha Sh.billioni 1.2 zimetengwa kuanzisha viwanda vidogovidogo.

Pia mikopo ya Wanawake,Vijana na walemavu,kiasi cha fedha Sh.Billioni 1.14 zimetengwa.

Ameongeza pia ukarabati wa Viwanja viwili vya Michezo na Uanzishwaji wa Meya Cup,Kiasi cha fedha Sh milioni 150 zimetengwa.

Wakati ununuzi wa magari na mitambo ya kisasa ya kuzolea taka na kusafisha Halmashauri ambapo kiasi cha Sh. bilioni 1.2 zimetengwa.

Jocob ametaja kipaumbele kingine ni ujenzi wa Ofisi za walimu kwa shule za sekondarI na Msingi,Kiasi cha Sh.milioni 300 zimetengwa.

Pia kipaumbele cha 11 ni kuboresha huduma za usambazaji wa maji safi na salama kwa wananchi,maeneo ya kwembe,kibamba,Goba,kimara,saranga,Mbezi na Msigani fedha Kiasi cha Sh.bilioni 1.303 zimetengwa kumaliza tatizo la Maji Ubungo.

Jacob amesema huduma za afya bure kwa wazee na upewaji wa Vitambulisho kwa ajili ya matibabu. Fedha kiasi cha Sh.milioni 60 zimetengwa.

Amesema kipaumbele cha 14 ni kuboresha huduma za ushauri na ugani kwa ufugaji na kilimo cha mjini,fedha kiasi cha Sh.milioni 120 zimetengwa.

Kipaumbele kingine ni uanzishwaji wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Ubungo,fedha kiasi cha Sh.milioni 100 kwa ajili ya utwaaji wa eneo la Hospitali na upembuzi yakinifu.

Jacob amesema pia uanzishwaji wa machinjio ya kisasa ya Nyama Halamshauri ya Ubungo,fedha kiasi cha Sh.milioni 150 zimetengwa.

Wakati kipaunbele cha 17,Jacob amesema ni uanzishwaji wa ujenzi wa masoko makubwa ya vyakula na Nafaka, Kibamba na Kwembe fedha kiasi cha Sh Milioni 450 ambazo zimetengwa.

“Kwa pamoja tujenge Halmashauri yetu kwa maslahi ya wananchi wetu,tutaendelea kusimamia maendeleo ya wananchi kwa kuhakikisha vipaumbele vyetu vinatekelezwa,” alisema Jacob.

No comments