KIONGOZI WA BAVICHA AACHIA NGAZI
Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Tanzania Bara, Getrude Kokwenda Ndibalema amejiuzulu wadhifa huo leo Machi 12, 2018.
Kupitia taarifa yake kwa umma aliyoitoa asubuhi ya leo, Ndibalema amesema amefikia uamuzi huo ili apate nafasi ya kufanya shughuli zake binafsi kulingana na taaluma yake kwa uhuru zaidi.
Amesema licha ya kujuzulu wadhifa huo, ataendelea kuwa mwanachama na mtanzania wa kawaida.
Ndibaleba alihudumu kwenye wadhifa wa Unaibu Katibu Mkuu BAVICHA Tanzania Bara katika kipindi cha miaka minne, kuanzia mwaka 2014 hadi Machi 11, 2018.
Na Regina Mkonde
Post a Comment